Brian na Mkude wapo kwenye basi. Wanasafiri kwenda Moshi.
Brian: Leo hali ya hewa ni nzuri sana.
Mkude: Ndiyo. Leo ni baridi kidogo. Jana ilikuwa joto kali sana. Lakini kwa kawaida wakati wa kiangazi jua ni kali.
Brian: Kiangazi kinaanza lini?
Mkude: Kiangazi ni mwezi wa kwanza na wa pili. Baada ya hapo ni masika. Masika ni msimu wa mvua nyingi sana. Msimu huu unaanza mwezi wa tatu mpaka mwezi wa tano. Wakati mwingine mvua za manyunyu huweza kuendelea mpaka mwezi wa sita. Wakati huu watu hufanya kazi mashambani. Wanapanda miche ya miti na matunda mbalimbali. Mazao ya chakula kama mahindi, mpunga, ngano na kadhalika hupandwa pia.
Brian: Mna misimu minagapi?
Mkude: Tanzania kuna misimu mine. Baada ya masika kuna msimu wa kipupwe tangu wezi wa sita mpaka mwezi wa tisa. Huu ni wakati wa vumbi, baridi kali na upepo mkali. Tena kuna sehemu ambazo baridi ni kali kuliko nyingine.
Brian: Na msimu wa nne je?
Mkude: Msimu wa nne ni ule wa vuli kutoka mwezi wa kumi hadi mwezi wa kumi na mbili. Huu ni wakati wa mvua ndogo na za muda mfupi. Wakati huu watu hupanda mazao ya muda mfupi kama maharagwe, viazi vitamu, viazi mviringo, mihogo, mtama, mboga za majani na kadhalika.
Brian: Ahaa! Asante sana kwa kunielimisha.
브라이언과 Mkude 버스에 있습니다. 담배를 여행.
브라이언 :. 오늘 날씨는
Mkude 아주 좋은 것입니다 : 예. 오늘은 조금 시원하다. 어제는 매우 뜨거웠다. 여름의 시작
Mkude 때 : : 여름이 새로운 제 1 및 제 2.하지만, 일반적으로 여름에는 태양이
브라이언 강하다. 그 후에는 후자입니다. 후자는 폭우의 계절입니다.이번 시즌 다섯 번째 달까지 3 개월 째 시작합니다. 때때로 소나기 6 월까지 계속 될 수있다. 이번에는 사람들은 농장에서 작동합니다. 그들은 다양한 과일 나무의 묘목을 심었습니다. 등등 옥수수, 쌀, 밀 등 식량 작물도 재배하지 않습니다
브라이언 :. 더 minagapi의 계절
Mkude : 탄자니아가 사계절.6-9개월이 없기 때문에 겨울 장마 후. 이것은 극도의 추위와 강한 바람 먼지하는 시간이다. 다시 겨울이 다른 것보다 더 온화 곳이 있습니다
브라이언 :. 제 4 절기는 당신을
Mkude은 : 네 번째 시즌 열 번째 달 두번째 달에 가을입니다. 이 작은 임시 비가 때입니다.사람들은 그래서 콩, 고구마, 감자, 카사바, 기장, 야채와 임시 작물 성장이 시간
브라이언 :. 오! kunielimisha 주셔서 대단히 감사합니다.
번역되고, 잠시 기다려주십시오..